Mpiganaji masumbwi, Francis Cheka amezungumzia suala la uchawi katika mchezo ndondi na kudai kuwa wapo baadhi ya wapiganaji ndondi wanaodai kuwa yeye ni mchawi na anapigana kwa ajili ya ushirikina.

Cheka amesema haamini kama uchawi upo kwenye ulingo ila anachokiamini ni kwamba uchawi upo nje ya ulingo”.

Amesema hayo akidai kuwa wapiganaji wengi wa ndondi hawapati sapoti kutoka kwenye makampuni kwa udhamini kama ilivyo kwa wasanii wa muziki.

“Wengi wanasema cheka mchawi anapigana kwa ajili ya ushirikina, ndondi hazina uchawi yani uchawi wa ngumi wanakuharibia maisha yako wewe ya nje ya ulingo” amesema Cheka.

Sikiliza hapa kinagaubaga Cheka alipofanyiwa mahojiano na chombo cha habari cha Dar 24.

JPM ampongeza IGP Sirro 'Unajitahidi'
Mpinzani atamba kushinda Urais DRC, Marekani yatuma jeshi

Comments

comments