Chama cha Social Democratic SPD kimepiga kura kuunga mkono kuanza kwa mazungumzo ya mwanzo ya kuunda  serikali ya mseto na chama cha kansela Angela Merkel.

Wajumbe wa chama cha SPD wamepiga kura 362 za ‘ndio’ dhidi ya kura 279 za ‘hapana” kusonga mbele na  majadiliano baada ya viongozi wa chama hicho cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto kukubali muongozo wa  muungano pamoja na kundi la vyama vya Kihafidhina vinavyoongozwa na Kansela  Merkel mapema mwezi huu.

Aidha, Mazungumzo yanatarajiwa kuanza wiki hii ili kuleta ahueni kwa washirika wa Ujerumani barani Ulaya ambako Merkel kwa muda mrefu amechukua nafasi ya uongozi katika masuala ya kiuchumi na usalama.

Hata hivyo, Kiongozi wa chama cha Social Democratic SPD, Martin Schultz katika hotuba yake kwa wajumbe aliwataka wanachama wa chama hicho kupiga kura kwa ajili ya kufungua mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha kansela Merkel, akisema serikali imara ya Ujerumani inahitajika kuimarisha Ulaya na kuwa kama ukuta dhidi ya siasa kali za mrengo wa kulia.

Video: Sam wa Ukweli afichua kilichomkuta hadi kuhamia kwenye kilimo
Chupi anasa mkoani Lindi