Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Ujerumani (SPD), Martin Schulz amesema kuwa anataka kujadili upya masuala muhimu ambayo awali yalikuwa yameshajadiliwa kati ya chama chake na vyama ndugu vya Kihafidhina vya CDU na CSU.

Ametoa kauli hiyo ya kurejea suala mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano ikiwa ni msimamo wake baada ya kupata uungwaji mkono kidogo kutoka kwenye chama chake cha SPD.

Schulz amesema kuwa atakutana na kiongozi wa chama CDU Kansela Angela Merkel na kiongozi wa vyama ndugu vya CSU, Horst Seehofer.

Aidha, Schulz ametilia mkazo msimamo wa chama chake kuwa mada muhimu zinazohusu masilahi ya jamii zitajumuishwa katika mazungumzo kabla ya kufikia makubaliano ya mwisho.

Hata hivyo Washirika wa kansela, Angela Merkel wanapinga mabadiliko yoyote kwenye makubaliano ambayo yalikuwa tayari yameshafikiwa katika mazungumzo ya mwanzo.

 

The Playlist ya Times FM yamtuza Vanessa Mdee ‘Plaque’ ya Nyota wa Mchezo
Peter Msigwa ashikiliwa na polisi atiwa mahabusu