Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametangaza kujiuzulu uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Kuyeko ambaye ni diwani wa Bonyokwa amesema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli Kwa kazi nzuri anazozifanya na kuwaomba Watanzania kumuunga mkono.

“Rais Magufuli ni mtu wa kuigwa, anastahili sifa na kazi ya kutukuka, nawaheshimu Viongozi wa CHADEMA kwa kunipa nafasi, nawashukuru na nitaendelea kuwaheshimu lakini mapenzi yangu ya dhati ni CCM” Amesema Kuyeko

Aidha, amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwani ameridhisha na utendaji kazi wa serikali ya Awamu ya Tano, hivyo hakuna budi ya kuendelea kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ameamua kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani ndicho chama kilichomlea na kumfikisha hapo alipo, hivyo anawashukuru sana viongozi wa Chadema kwa ushirikiano wao waliompatia wakati wa uongozi wake.

 

Video: ACT- Wazalendo, Chadema vita mpya, CUF yapukutika Zanzibar
CUF yajikabidhi mikononi mwa CCM,'Huwezi kumdharau kiongozi wa CCM'

Comments

comments