Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaanza kufanya mikutano ya hadhara kwa kile walichokidai kuwa walikuwa wanakabiliwa na mambo mengi ndani ya chama hicho.

Hayo yamesemwa jijijni Dar es salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vincent Mashinji ambapo amesema kuwa awali walionekana kutii agizo hilo la katazo ya mikutano ya kisiasa kwa sababu chama hicho kilikuwa kinashughulika na ujenzi wa chama chake.

“Ni kweli tulikuwa na jukumu la ujenzi wa chama kama taasisi, kwa hiyo tulikuwa hatuna uwezo wa kuendesha vitu viwili kwa wakati mmoja, ndiyo maana wakati tamko linatokea na matendo yetu ilionekana kutii amri isiyokuwa halali bali ni matukio mawili ambayo yaliyotokea kwa wakati mmoja na moja kumeza jingine.” amesema Mashinji.

Aidha, kuhusu na Uchaguzi wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Katibu Mkuu huyo amesema kupitia kamati kuu wameandaa mikakati ambayo itawafanya kuibuka na ushindi.

Akipokea ripoti ya Tume ya Taifa Uchaguzi NEC, June 07, 2016 Rais Magufuli aliwataka viongozi wa kufanya siasa hadi 2020, lakini kwa sasa wawape nafasi viongozi waliochaguliwa kutekeleza waliyoyaahidi.

Zaidi ya watoto 100,000 hufariki kwenye vita kila mwaka
Manispaa ya Ilala yatoa mkopo wa shil. mil. 153 kwa vikundi

Comments

comments