Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha mikutano yote ya chama hicho ambayo awali alitangaza kuwa ingefanyika nchi nzima kuanzia April 4, 2020 mwaka huu.

Mara baada ya kutoka gerezani Machi 16 Mbowe alitangaza kuwa Chadema itafanya mikutano nchi nzima kuanzia Aprili 4, 2020 ili kudai tume huru ya uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

Leo Machi 23, 2020 jijini Dodoma, Mbowe ameomba wanachama wa chama hicho kushirikiana na watanzania wote bila kufanya mambo ya siasa ili wapambane katika vita ya kupambana na virusi vya Corona.

Hayo yamejiri huku tanzania ikiwa na visa 12 vya wagonjwa waliokutwa na virusi hivyo ambapo mgonjwa wa kwanza Tanzania kuthibitika na ugonjwa  huo akiwa hana tena virusi hivyo.

 

Halima Mdee, Ester Bulaya kizimbani kwa kufanya vurugu Segerea
Video: NEC yatangaza tarehe uboreshaji daftari awamu ya pili

Comments

comments