Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetetea sababu ya wabunge wake kutoonekana kwenye baadhi ya shughuli za Maendeleo kwa kile walichokidai kuwa wabunge wake hawakupewa mialiko na wengine wakiwa na kesi mbalimbali mahakamani.

Hayo yamejiri mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kusema kuwa wabunge wa upinzani hawaonekani kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema kuwa Makonda amesahau sana kuwa wabunge wao walifukuzwa katika ofisi zao za kinondoni na kumtaka aeleze anakopelekaga mialiko hiyo.

“Nashangaa hata wale wabunge wapinzani wa Dar es salaam ambao mara nyingi wanakuja vyuoni kuwarubuni wanafunzi wawapigie kura lakini hawatokei kwenye shughuli za maendeleo, kazi yao ni kukosoa tu,”amesema Makonda

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakijionyesha kuwa ni wapiganiaji wa maendeleo kwa maneno na sio vitendo, huku akimpongeza Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa kwakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono wa shuguli mbalimbali za maendeleo.

Juan Cuadrado ahimiza ushindi Juventus FC Vs Valencia CF
RC Mndeme afuta likizo za watumishi