Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji wametofautiana kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema ambapo amesema kuwa hakuna kikao chochote cha Kamati Kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, si tu nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe bali popote pale.

“Tunaomba Watanzania na wanachama wetu wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao,”amesema Mrema

Amesema haijawahi kutokea wakati wowote vikao vya kamati kuu vikafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa taifa wa chama hicho kama ambavyo taarifa hizo zinadai.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni CHADEMA imekumbwa na wimbi la hamahama ya wabunge wake na kujiunga na CCM, huku sababu kuu inayotajwa na viongozi hao wanaojiuzulu ni migogoro ndani ya chama hicho inayosababishwa na mwenyekiti Freeman Mbowe.

Trump adai huenda mwandishi aliyetoweka aliuawa na Wahuni
Rais Museveni awapa Kanye West, Kim Kardashian majina ya Kiganda