Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazoendelea kuzagaa mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene amesema kuwa taarifa hizo si za kweli.

Amesema kuwa Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote juu ya kurejea kwake nyumbani kwa sababu zilizo wazi kwamba bado hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwisho wiki hii au wiki ijayo.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa tatizo hilo kupuuza taarifa hizo.

Hata hivyo, Tundu Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu baada ya kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari.

 

Mkuu wa shule mbaroni kwa ubakaji
Arjen Robben kuikosa Real Madrid kesho