Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimezuiliwa kufanya mikutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, kwenye jimbo la mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mikutano wilayani humo.

“Nimeagizwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Hai. nikuandikie kukutaka kusitisha mikutano na ziara ya viongozi wako kitaifa, tarehe 29/12/2018 na kuendelea”, imesema barua hiyo.

Hata hivyo, baada ya zuio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amethibitisha kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine watatu kwa makosa ya kufanya kusanyiko bila kibali.

Aussems ajipa matumaini michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Video: Magufuli aibua mkanganyiko mpya, Vigogo walioonja joto la jiwe 2018