Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt.Bashiru Ally amesema chama hicho hakitatoa tisheti za bure kwa wanachama wake Uchaguzi Mkuu ujao 2020, na kuwataka wanachama wajinunulie wenyewe.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akiwa mkoani Kagera ambapo amesema maelekezo hayo ni kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa kwani wamejipanga kutumia gharama ndogo kwenye Uchaguzi ujao.

amesema kuwa “matarajio yangu uchaguzi ujao tutatumia pesa kidogo, na tumeshasema hatutanunua tisheti za kuwagaiwa wanachama wakati wa Uchaguzi”

Na kusisitiza “Hakuna cha bure, kwakweli hakuna cha bure kama Makao Makuu wanachapisha tisheti kuwapa wanachama maanayake wameomba kwa Matajiri”.

Kakolanya ampindua Manula Simba
Video: Makamba" Nimechoka yanayoendelea", Bashiru atishia kuwafukuza wavurugaji CCM