Zikiwa zimebaki siku 38 kabla watanzania hawajapiga kura ya kumchagua rais wa serikali ya awamu ya tano, vyama viwili ushindani zaidi vya CCM na Chadema inayoungwa mkono na Ukawa wamejinasibu kwa nyakati tofauti kuwa tafiti walizofanya zinaonesha wameshinda.

Akiongea na kituo cha runinga cha East Africa TV, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba alieleza kuwa tafiti zilizofanywa na chama hicho kwa njia ya kidijitali zimeonesha kuwa mgombea wake John Magufuli anaongoza kwa asilimia 69.3.

“Ukweli ni kwamba tunafanya vizuri, na uthibitisho wa hilo ni kwamba tumefanya utafiti wetu wa ndani wa kura za maoni wa chama na mpaka sasa tunaongoza kwa asilimia 69.3 na Imani yetu ni kwamba mgombea wetu atakapomaliza kampeni basi asilimia hizo zitakuwa zimeongezeka,” alisema Makamba.

Wakati makamba akijigamba kwa utafiti wa chama chake, mwenyekiti mwenza wa Ukawa jana alieleza kuwa ngome hiyo imefanya utafiti wa ndani na kujiridhisha kuwa mgombea wao, Edward Lowassa anaongoza katika kinyang’anyiro hicho kwa asilimia kubwa.

Hata hivyo, tafiti za pande hizi sio tafiti rasmi hivyo watanzania wanasubiri kusikia matokeo ya awali ya tafiti zilizofanywa na taasisi za Twaweza na IPSOS – Synovet kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Taasisi hizo zinatarajia kutoa matokeo ya tafiti zake mapema wiki ijayo.

CCM Wanamtaka Lowassa...
Rais Kikwete Atembelea Kituo Cha Michezo Cha Kidongo Chekundu