Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao hiyo kwa kuwachonganisha baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itifaki na Uenezi, Humphrey Polepole imesema kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Bashiru Ally hana akaunti ya mtandao wa kijamii ‘Twitter’

Taarifa hiyo iliyotolewa imeeleza kuwa watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuhusu chama hicho, wana lengo la kuleta taharuki ndani ya chama hicho.

“Jana katika mitandao ya kijamii, watu wenye hila, fitna, husuda na kila dalili za uzandiki, wametengeza kauli ya kubeza, potofu, kwamba Dkt. Bashiru Ally kamjibu kiongozi mstaafu Pius Msekwa,”imeongeza taarifa hiyo

Hata hivyo, katika taarifa hiyo, Polepole amekanusha taarifa zilizokuwa zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kutakuwepo mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Lumumba jijini Dar es salaam.

Video: Cardi B aachana na mumewe Offset
Hii hapa siri ya ushindi kwa Queen Elizabeth Miss World 2018

Comments

comments