Kamati ya siasa ya Wilaya ya Muleba imewajulisha wananchi rasmi kuwa Chama cha Mapinduzi CCM, hakihusiki na tuhuma za kutekwa kwa mgombea wa udiwani wa Chadema kata ya Buhaganza, Nelson Athnas ambaye alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakihusiki kwa lolote lile na tuhuma hizo zinazoongozwa na viongozi kwa nia mbaya ya kuwachafua na kukichafua chama na kuvuruga uchaguzi baada ya kuzidiwa” amesema Tibaijuka.

Tibaijuka amesema kuwa CCM imejitayarisha vyema kwa ushindani na inaamini mgombea wake Bi. Jenitha Tibihenda anatosha hivyo amedai kuwa hakuna haja ya kumteka mshindani wake yoyote.

Aidha Tibaijuka alivitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa tukio hilo kwa haraka ili watu waliotenda tukio hilo ovu waweze kupatikana kwa haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mgombea wa udiwani Kata ya Buhangaza, hanasio Makoti aliyekuwa amepotea tangu Februari 2, 2018 alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui, CHADEMA imesema alitupwa barabarani maeneo ya Hospitali ya Kagondo na sasa aendelewa kupatiwa matibabu.Muleba (CHADEMA), At

Aliyemuua Bob Marley ajitokeza, adai kutekeleza mpango wa Marekani kuwaua...
Seedorf achaguliwa kuwa kocha mpya Deportivo