Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuzibomoa ngome za mpinzani wake mkuu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika chaguzi za marudio, ambapo jana mgombea wake wa udiwani kata ya Turwa, Tarime Mjini mkoani Mara aliibuka kidedea.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo wa marudio alimtangaza Chacha Mwita kuwa mshindi akipata kura 1,401 dhidi ya mgombea wa Chadema, Charles Mnanka aliyepata kura 1,121.

Matokeo hayo yamemaliza mbio za uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali kutokana na mji huo kuwa moja kati ya ngome za Chadema ikiwa chini ya Mbunge wa chama hicho, Esther Matiko. Chadema wameshindwa kutetea kiti hicho cha udiwani kupitia kura 2,539 zilizopigwa, huku NCCR-Mageuzi wakiambulia kura 17 tu.

Hata hivyo, matokeo hayo hayakupokewa mikono miwili na Chadema ambao walikuwa wakishangilia muda wote wakiamini mgombea wao ameshinda kwa kishindo lakini matokeo rasmi yalisitisisha furaha yao.

Chadema wakiongozwa na Katibu wa mkoa wa Mara, Chacha Heche wamepinga matokeo hayo wakidai yamechakachuliwa na kwamba mgombea wao ndiye mshindi. Viongozi hao hawakuweka wazi kama watafuata taratibu za kisheria kupinga matokeo hayo mahakamani au la.

Ushindi wa CCM kwenye kata nyingine ni pamoja na Kaloleni Arusha Mjini, Songoro na Makorora mkoani Tanga.

Ushindi mzito wa CCM ni katika katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Buyungu mkoani Kigoma ambapo Christopher Chiza  alimwaga Elia Michael wa Chadema.

Mfanyakazi aiba ndege Bombardier Q400, aiangusha
Video: Vurugu zatawala uchaguzi Arusha, Kubenea afunguka kuhamia CCM