Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi safu ya kikosi cha makada wakongwe wa chama hicho watakaokuwa msitari wa mbele kumpigia debe mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli huku kikitarajiwa kumuangamiza kisiasa mgombea wa Chadema, Edward Lowassa.

Chama hicho kilitangaza rasmi jana Kamati yenye wajumbe 32, wengi wao wakiwa makada waliowahi kuwa maadui wa kisiasa wa Edward Lowassa wakati akiwa CCM huku ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulahman Kinana.

Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alikiri kuwa na adui wa Lowassa kwa kipindi cha miaka 12 aliyatakaja majina ya wajumbe wa kamati hiyo na kueleza kuwa watafanya operesheni kila siku katika maeneo mbalimbali nchini.

“Kamati Kuu ya Kampeni ya CCM ni Kamati Kuu ya Taifa ya chama, lakini kamati itakayokuwa ikifanya operesheni ya kila siku ni hii niliyoisoma hapa na itakuwa chini ya Abdulrahaman Kinana na Makamu wenyeviti wawili, mmoja Tanzania Bara na nyingine Tanzania visiwani,” alisema Nape huku akisisitiza kuwa kutakuwa pia na kamati nyingine ndogondogo zitakazoisaidia kamati hiyo katika ngazi za mikoa.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ni wale waliokuwa kwenye mbio za urais wakati wa kura za maoni za chama hicho na wengine walikuwa katika timu ya kampeni ya Edward Lowassa wakati akiwa CCM akiwania nafasi ya kugombea urais kupitia chama hicho na baadae jina lake kukatwa.

Wajumbe wa kamati hiyo inayoongzwa na Abdulrahaman Kinana ni pamoja na Rajab Luhwavi, Vuai Vuai, Abdalla Bulembo, January Makamba, Mwigulu Nchemba, Asha Rose Migiro, Samuel Sitta, Rajab Luhwavi, Dk. Harrison Mwakyembe, Lazaro Nyalandu, Stephen Wasira, Bernard Membe, Makongoro Nyerere, Christopher Ole Sendeka, Sadifa Juma Khamisi, Shamsi Vuai Nahodha, Sophia Simba, Livingstone Lusinde, Anthony Dialo, Ummy Mwalimu, Steven Masele na Pindi Chama.

fimbo

Wajumbe hao walianza kutamba kuwa watahakikisha wanamletea Dk. Magufuli ushindi wa kishindo wa kishindo kwa kuwa kushindana naye huku wakiifananisha timu ya kampeni ya Lowassa kama timu ya daraja la tatu na wao ni Arsenal.

Kipenga cha kuashiria kuanza kampeni kitapulizwa rasmi na tume ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Agosti 22 mwaka huu.

Maradona Amzawadia Muamuzi Wa Mkono Wa Mungu
Ali Kiba Na Neyo, Kazi Imeanza