Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe mkoani Njombe kimeazimisha miaka 42 tangu kuanzishwa kwa chama hicho kwa kupanda miche ya Chai na wananchi wa Kijiji cha Uliwa Kata ya Ihungilo mkoani humo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Njombe, Hitla Benjamini Msola amesema kuwa chama hicho kimeamua kufanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho ili kuakisi ukombozi wa uchumi wa Tanzania.

“Kwanza tumefikisha miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi, na huko nyuma tulikuwa tukiadhimisha kwa ngonjera na nyimbo lakini kwa sasa tuko na (CCM) mpya inayofanya kazi kwa vitendo na tumeamua kufanya hivi na kufanya kazi ambazo,”amesema Msola

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Elnest Ngaponda amewataka wakulima wa chai kuonyesha juhudi katika kilimo hicho kwa kuwa kitakuwa na uhakika wa kipato ukilinganisha na mazao mengine ya viazi na mahindi.

Naye Meneja wa Kampuni ya NOSC, Philibet Kavia amesema kuwa wataendelea kumsaidia mkulima wa chai licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundombinu.

Hata hivyo, zaidi ya miche 12600 ya chai imepandwa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi katika shamba la moja ya kikundi cha wakulima kijijini hapo katika maadhimisho ya miaka 42 ya chama cha mapinduzi yaliyofanyika katika Kata ya Ihungilo.

UVCCM Njombe kuitisha mkutano wa vijana kuhusu sakata la mauaji
JPM azindua Mahakama inayotembea ya Sh470 Milioni, atoa neno