Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya viongozi wa wake wa serikali za mitaa wasiowajibika kusoma mapato na matumizi huku chama kikiahidi kutowarudisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa  mwaka 2019.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho,  Humphrey Polepole wakati akiwa katika ziara ya Kata kwa kata ya uhuishaji wa hai wa Chama na ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha Mjini katika Kata za Engutoto, Lemara, Muriet, Terrat, Olasiti na Osunyai.

Amesema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa viongozi wote wasiowajibika, wasio soma mapato na matumizi kwa mujibu wa sheria, wenye tabia za kupokea au kutoa rushwa Chama hakitawavumilia na hawatapewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

“Tunaposimamisha wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 tunahitaji watu mwenye tabia nzuri, waaminifu, wanyenyekevu, wachapakazi, wapole lakini wakali kwenye mambo ya hovyo na wanaokubalika kwa watu” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha, akiwa katika ziara hiyo Polepole amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) la hospitali ya Wilaya ya Arusha Jiji lililopo katika Kata Engutoto, Ujenzi wa barabara kuu ya mchepuko (kilometa 42. 4 kwa kiwango cha lami) yenye madaraja 7, ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Terrati katika Kata ya Muriet, Ujenzi wa madarasa manne katika shule ya msingi muriet Darajani na ujenzi wa barabara ya Sombetini FFU yenye urefu wa kilometa 2.1 kwa kiwango cha lami.

 

Trump uso kwa uso na Kim Jong Un
Ajali mbaya yatokea Mjini Bukoba