Mbio za uchaguzi Mkuu zimefika mahala pake baada ya chama tawala (CCM) kuanza kurusha kete yake kwa mara ya kwanza, ambapo jana maelfu ya wananchi walifurika katika viwanja vya Jangwani kushuhudia uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Samiah Suluhu Hassan alipata nafasi ya kuwahutubia watanzania na kukinadi chama hicho pamoja na mgombea urais Dk. John Pombe Magufuli.

Katika ahadi zake, Bi. Samiah alisema kuwa endapo wananchi watakipa ridhaa chama hicho, kitatoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo ya kila kijiji. Pamoja na ahadi hiyo, aliongeza kuwa wanawake watafaidika zaidi kwa kukichagua chama hicho kwa kuwa kitaimarisha vikundi vya akina mama vikiwemo VICOBA.

Alisema kwa mujibu wa ilani yao watahakikisha wanaboresha huduma za afya hasa vijijini. “Kila kijiji kitakuwa na kituo cha afya,” alisema.

Aidha, Bi. Samiah alisema kuwa wakipewa ridhaa ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, watahakikisha wanatatua tatizo la vifo vya kina mama wakati wa kujifungua na kutatua tatizo la mimba zisizotarajiwa, “zile mimba tusizozitarajia hatuzipendi.”

Mwinyi Aivuruga Ukawa, Kauli za Mkapa Zawapa Ukawa 'Point' Ya Kuanzia
Kitendawili Cha Dk. Slaa Kuhudhuria Uzinduzi Wa CCM Chateguliwa