Kiungo kutoka nchini Brazil Carlos Henrique Casimiro (Casemiro), amesema hatua ya kufungwa na Atletico Madrid katika mchezo wa UEFA Super Cup usiku wa kuamkia leo, isimuhusishe aliyekua mshambuliaji wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo aliyejiunga na mabingwa wa soka Italia Juventus.

Casimiro amesema suala la kufungwa katika mchezo huo ni la kawaida, na alihusiani na mchezaji yoyote kuwepo ama kutokuwepo, hivyo ameshauri ushindi wa Atletico Madrid uheshimiwe.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, amesema itakua upuuzi na ujunga kama mtu wa Real Madrid atajitetea kwa jina la Ronaldo ambaye kwa sasa hayupo kwenye kikosi.

“Kufungwa ni sehemu ya mchezo, Ronaldo alikuwepo hapa na tuliwahi kupoteza, siamini kuondoka kwake imekua sababu ya sisi kupoteza mchezo wa leo (Jana)” Alisema Casemiro.

“Suala la msingi ni kuheshimu ushindi walioupata wapinznai wetu, ninaamini umetokana na makosa tuliyoyafanya katika muda wote wa dakika 120 tuliocheza”

Baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wakiwa katika hali ya majonzi kufuatia kufungwa na Atletico Madrid mabao manne kwa mawili usiku wa kuamkia leo.

“Ronaldo atabaki katika historia ya klabu ya Real Madrid, kwamba aliwahi kupita hapa na akacheza kwa mafanikio makubwa, suala la kufungwa kwa sasa ama kushinda halitomuhusu”.

Katika mchezo huo wa UEFA Super Cup Real Madrid walikubali kibano cha mabao manne kwa mawili na kushuhudia majirani zao Atlertico Madrid wakitwaa ubingwa wa mchezo huo ambao ni maalum kwa ufunguzi wa msimu wa michuano ya Ulaya.

Mabao ya Atletico Madrid katika mchezo huo yalifungwa na Diego Costa dakika ya 1 na 79, Saul Niguez dakika ya 99 na Koke dakika ya 104, huku mabao ya kufutia machozi kwa mabingwa wa soka barani Ulaya yakipachikwa wavuni na Karim Benzema dakika ya 27 na Sergio Ramos kwa njia ya mkwaju wa Penati dakika ya 63, baada ya beki wa Juafran kuunawa mpira katika eneo la hatari.

TACIP yazidi kupeta, wasanii waanza kupatiwa elimu
Ufaransa yashika usukani viwango vya ubora duniani