Mke wa waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau, bi Sophie Gregorie Trudeau, amethibitishwa kupona ugonjwa wa covid 19 baada ya kuumwa kwa takribani siku 27.

Kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika ” najisikia vizuri sana na nimepokea majibu ya uthibitisho kuwa nipo salama kutoka kituo cha afya cha Ottawa”

Ameongeza kuwa ” kutoka ndani ya moyo wangu nataka kusema asante kwa kila mmoja ambaye alinijulia hali na kunitakia kila la heri”

Sophie alithibitika kuwa ameathirika na virusi vya covid 19 Machi 12, 2020 baada ya kurejea nchini kwao akitokea Britain, ambapo yeye pamoja na mume wake waliamua kujiweka karantini.

Idadi ya wagonjwa wa Corona Tanzania yaongezeka na kufikia 19
Rwanda kinara idadi ya waathirika wa Corona Afrika Mashariki