Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema kuwa uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoshirikiana na CAG, Profesa Mussa Assad utaligharimu taifa.

Utoh amesema kuwa ni vyema suala hilo likatazamwa kwa upana wake ili lisifike hatua ya kuligharimu Taifa.

“Kama Bunge limepitisha azimio la kutoshirikiana na CAG, hilo litakuwa tatizo kubwa hususan kwenye suala la uwazi,” Citizen imemkariri Utouh.

Hata hivyo, Utoh ambaye alishika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi kabla ya Profesa Assad amesema kuwa hawezi kutoa maelezo mengi zaidi kwa kuzingatia uzito wa suala husika.

Jana, Bunge liliazimia kuwa halitashirikiana na CAG kutokana na kile lilichoeleza kuwa Kamati ya Bunge ilimhoji na kujiridhisha kuwa msomi huyo hakuwa tayari kubadili msimamo wake wa dhidi ya kauli yake ‘Bunge ni dhaifu’.

CAG alitoa kauli hiyo mwaka jana alipokuwa nchini Marekani akifanya mahojiano na redio ya kimataifa kuhusu jinsi ambavyo Bunge limeifanyia kazi ripoti yake.

LIVE: Rais Magufuli akihutubia katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara
Serikali yawaonya wenye tabia ya kutumikisha watoto

Comments

comments