Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameripoti rasmi ofisini kwake leo Novemba 5, 2019 na kukabidhiwa ofisi na CAG mstaafu Prof. Mussa Assad.

Katika makabidiano hayo, Assad amesema kuwa ofisi hiyo ni Taasisi na kwa mujibu wa sheria, makabidhiano ya taasisi hufanywa kwa maandishi hivyo watakamilisha makabidhiano hayo kwa maandishi Makao Makuu Jijini Dodoma.

ameongeza kuwa ” Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wetu kazi basi anisamehe na mimi kuna mambo alinikosea nimemsamehe”.

Kwa upande wake CAG kichere amesema kwakuwa tayari anajua ugumu wa kukusanya mapato alioupata akiwa TRA, atalinda mapato ya serikali kwa wivu mkubwa .

” Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya” amesema Kichere.

Ameongeza kuwa katika nafasi hiyo aliyopewa atahakikisha ameimarisha mahusiano baina ya ofisi yake na Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama yalikuwa hafifu na atafanya mabadiliko kwa umakini mkubwa bila kuharibu mfumo wa utendaji kazi.

” Kama kulikuwa na mahusiano hafifu nitaimarisha mahusiano kati ya ofisi ya CAG na Bunge. kama kutakuwa na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa ili tusiharibu mfumo wa utendaji kazi.

Video: Harmonize aachia "Uno", Tazama hapa
UN yatuma misaada ya dharura Somalia