Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad ametoa Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Taarifa za Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

CAG ametoa ripoti hiyo leo Aprili 10, 2019 jijini Dodoma ambapo ameeleza kuwa masharika 14 ya umma yana hali mbaya kifedha na kusababisha madeni makubwa zaidi ya mitaji yao.

Ameongezea kuwa kati ya mashirika hayo, mashirika 11 yanajiendesha kwa hasara kwa miaka inayozidi miwili sasa.

Ametaja baadhi ya mashirika hayo ni shirika la ndege la Tanzania (ATCL), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Pesa), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Benki ya TWB.

“Mashirika 14 ikiwemo ATCL na Benki TWB yana matatizo kifedha na kusababisha kuwa na madeni makubwa kuliko mtaji wake” amesema CAG.

Aidha, katika ripoti yake amesema deni la taifa limeongezeka kutoka trilioni 46.08 kwa mwaka kufika trilioni 50.92 huku deni la ndani likiwa shilingi 14.73 na deni la nje likiwa trilioni 36.19 likiwa limeongezeka kwa asilimia 10.

CAG atoa msimamo neno 'dhaifu' litaendelea kutumika
LIVE: Rais Magufuli akizindua ujenzi wa barabara Njombe - Moronga

Comments

comments