Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), limepanga kutoa dola 200,000 kwa wanachama wake katika kusaidia kukabiliana na anguko la kiuchumi lililotokana na madhara ya COVID 19.

Kiasi hicho ni zaidi ya shilingi za Tanzania, milioni 460.

CAF pia inaangalia uwezekano wa kuyapa fedha mashirikisho na vyama vya soka vya kitaifa ambavyo vitapambana kuhakikisha wanamalizia misimu yao ya mashindano ya 2019/20.

Majuma mawili yaliyopita CAF ilitangaza mgao wa dola milioni 3.5 zitakazogawanywa kwa vilabu vinavyoshiriki mashindamo ya Afrika katika msimu huu wa 2019/20.

Mwezi uliopita, FIFA nao walikubali kutoa dola bilioni 2 zitakazogawanywa kwa wanachama wake (kila mmoja dola laki 5) kusaidia kupambana na anguko la uchumi lililosababishwa na virusi vya Corona.

Lakini mpango kamili wa FIFA ni kutoa dola milioni 1.5 kwa kila nchi mwanachama wake.

Hii ina maana kwamba Tanzania itapata dola milioni 1.7 kutoka mashirikisho makubwa ya kimataifa FIFA na CAF. Yaani dola laki 2 za CAF, dola milioni 1.5 za FIFA, zikitangulia dola laki tano halafu zitakuja dola milioni moja. Hii ni takribani shilingi bilioni 3 za Tanzania.

Zitto kutumikia kifungo cha kutotoa matamshi ya uchochezi mwaka mmoja
ASFC: Azam FC mdomoni mwa Simba SC