Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa ufafanuzi juu ya kauli aliyoitoa Spika wa Bunge, Job Ndugai bungeni kuhusu malipo ya ndege ambayo ilitumika kumsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Taarifa ya hiyo ya Bunge imesema kuwa watu wanaosema Spika wa Bunge amedanganya bunge si sahihi kwani wao wanadai Job Ndugai alieleza kuwa taratibu zote za ndege iliyomsafirisha Tundu Lissu iliratibiwa na Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Hassan Turky na bunge kusaidia.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na zinazoelezwa na baadhi ya wanasiasa kwamba Spika amewaongopea Watanzania si za kweli kwani taratibu zote zilizofanyika ziliratibiwa na kamishna wa tume ya utumishi wa bunge. Salim Hassan Turky ambaye ndiye aliyechukua dhamana ya safari hiyo.

Vile vile taarifa hiyo imeongeza kuwa ndege hiyo ilikuja kwa mkopo ambao ulidhaminiwa na mheshimiwa Turky ambapo deni hilo limelipwa leo mchana mara bada ya Spika Ndugai kutoa kauli hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa inawaomba wanasiasa ambao hawajui ukweli kuhusu jambo hilo waliache bunge liendelee kushirikiana na familia ya Mbuge huyo aliyepata matatizo pamoja na uongozi wa kambi rasimi Bungeni.

Kubenea augua ghafla Dodoma
Video: Vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni vyanena makubwa