Bunge nchini Agentina limeukataa mswada wa sheria ya kuruhusu  utoaji mimba zenye umri chini ya siku 15.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya malumbano ya hoja ya muda mrefu yaliyoafikia ukingoni kwa kuupigia kura mswada huo uliowasilishwa bungeni. Wabunge 38 walipiga kura ya kuukataa huku wabunge 31 wakipiga kura ya kuukubali.

Waandamanaji wanaopinga na wale wanaounga mkono walifurika nje ya bunge la nchi hiyo wakisubiri matokeo kuhusu muswada huo.

Wanaharakati wanaopinga utoaji mimba wameeleza kuwa, “ni furaha kuona jamii inaweza kukataa na kusimamia misingi muhimu ya kuwalinda wasio na uwezo wa kujilinda, hususan watoto wachanga.”

Kwa mujibu wa sheria zilizopo, ni kosa kutoa mimba isipokuwa kwa waliobakwa na kuthibitisha pamoja na sababu za kiafya za kumlinda mama dhidi ya hatari ya kupoteza maisha kutokana na ujauzito.

Matokeo hayo yalisababisha baadhi ya waandamanaji waliokuwa wanaunga mkono muswada huo kuanza kufyatua baruti kuelekea kwa askari polisi.

Bunge lilipata nafasi ya kuupigia kura muswada huo, baada ya Rais Mauricio Macri anayefahamika kwa kupinga utoaji mimba, kuruhusu ufikishwe bungeni na bunge liamue hatma yake.

Esther Matiko na wafuasi 15 wa Chadema waachiwa kwa dhamana
Gari la Mbunge wa Chadema lapata ajali mbaya