Bunge la China kwa mara nyingine limemchagua Xi Jinping kutalawa nchi hiyo kama Rais bila kikomo na limemteua Xi Ally kuwa makamu wake.

Rais Xi Jinping mwenye umri wa miaka 64 anatajwa kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa zaidi baada ya alieyekuwa kiongozi wa kihistoria wa nchi hiyo Mao Zedong.

Bunge hilo lilipiga kura na kufanya baadhi ya marekebisho ya katiba na kuondoa ukomo wa Rais wa kukaa madarakani.

Sheria hiyo imepitishwa na wabunge 3000 waliopiga kura na matokeo yalivyotolewa kura 2998 walipitisha pendekezo hilo kwa jibu la Ndio huku wabunge wawili tu ndio walipitisha kura ya Hapana.

Hapo awali katiba ya China ilikuwa inamruhusu Rais kukaa madarakani kwa kipindi cha mihula miwili tu huku kila muhula akitumikia kwa miaka 5 kama ilivyo katiba ya Tanzania.

Mwezi uliopita chama cha kikomunisti  cha China kinachoongoza taifa hilo kilitoa pendekezo la kubadilisha katiba juu ya ukomo wa Rais na makamu wa Rais, na leo wamethitisha kwa kupiga kura na pendezo hilo kushinda kwa asilimia 99.9.

 

Makonda awapa kibali wasanii kurekodi kazi eneo lolote
Prezzo afunguka kutompost Amber Lulu kwenye ‘birthday’ yake