Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umebadili mfumo wa utendaji kazi kwa kunzisha mtambo mpya utakaokuwa unachenjua mabaki ya awali kwa kutumia kemikali ya Syanaidi (Cyanide)

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Mawasiliano kutoka Acacia, Asa Mwaipopo wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi 2000 waliopunguzwa katika mgodi huo mara baada ya kushuka kwa uzalishaji.

Amesema kuwa mtambo huo mpya wa uzalishaji ambao utatumia kemikali Sayanaidi utasaidia kuzalisha ajira 150 ndani ya Kampuni hiyo, huku wakiajiri wafanyakazi wengine 150 kwaajiri ya kufanya usafi na ulinzi mgodini hapo.

Naye Mwakilishi wa chama cha wafanyakazi, Kazimili Lubigisa amesema kuwa kufungwa kwa mtambo huo kumesababisha madhara makubwa kwa wafanyakazi na Serikali kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na familia zao kuathtirika kiuchumi, afya na kisaikoloji.

Hata hivyo, kwa upande wake Meneja wa mgodi huo anayeondoka nchini baada ya kufanyakazi kwa muda wa miaka miwili, Graham Crew amesema kuwa hakuna mtu anayefurahia hali hiyo na amewataka wafanyakazi hao kuwa na imani na mazungumzo yanayoendelea baina ya serikali na mgodi huo kuwa yataleta muafaka ili kuendelea na uzalishaji.

 

 

Van Nistelrooy amtabiria makubwa Lukaku
RC Gambo apiga marufuku viongozi kukamata watumishi