Wabunge  nchini Bukina Faso wamepitisha Muswada utakaowezesha wananchi kupewa silaha ili kupambana na Makundi ya waasi na Muswada huo unalengo la kupunguza mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya Al-Qaeda na Islamic State.

Kwa mujibu wa wabunge hao, uwezo wa Jeshi kupambana na wanamgambo hautoshi kutokana na idadi yao kuwa ndogo lakini pia hawana mafunzo ya kutosha.

Wakosoaji wamehoji ikiwa hatua mpya itawafanya watu waumie lakini Serikali inasisitiza kuwa, watu watakaojitolea kuwa na silaha ni muhimu kwani watasaidia kumaliza ghasia.

La Liga wataja muda wa kuanza kwa El Classico mzunguuko wa pili
Mvutano waibuka Bungeni sheria ya wabakaji kuhasiwa