Ni siku nyingine, ni mafanikio mengine kwa klabu ya Singida United kuingia mkataba mnono wa miaka miatatu (3) wa kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV kupitia Azam Tv.

Akizungumza kwa furaha, Mkurugenzi wa Singida United Football Club Ndg. Festo Sanga amesema “tunawashukuru Uhai production wanaoendesha Azam Tv kwa kukubali kuanzishwa kwa kipindi cha Singida United Tv kitakachokuwa kinarushwa kupitia Azam Tv.”

“Ni mafanikio ya kujivunia kuona kila mkakati tunaoupanga unafikia malengo, tunaendelea kuwaomba watanzania na wadau wa mpira kuwa tuungane kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu vyetu na zaidi soka kwa ujumla. “Pia kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV ni moja ya njia ya kuwatangaza wadhamini wetu ambao wamewekeza kwenye club yetu.”

Pichani ni CEO wa Uhai Production Ndg. Tido Mhando akimkabidhi mkataba walioingia leo ndg. Festo sanga Mkurugenzi wa Singida United Football Club.

Tanzania yakanusha vikali kuwa na uhusiano na Korea Kaskazini
Korea Kaskazini yafyatua kombora jingine, Japan yalalama