Uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspur inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza umemtangaza, Jose Mourinho kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.

Akizungumzia uteuzi huo mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amesema Mourinho ni kocha mwenye mafanikio kwenye soka, hivyo wanaamini atawasaidia.

”Uzoefu wake na mbinu zake ni chachu ya mafanikio aliyoyapita katika klabu alizozinoa na tuna amini ataleta hamasa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo,” alisema Levy.

Kuteuliwa kwa Mourinho kuinoa Spurs kumefuatiwa na kutimuliwa kwa aliyekua kocha wa awali wa timu hiyo, Maurico Pochetino ambaye alidumu klabuni hapo kwa muda wa miaka mitano.

Pochetino ameiongoza timu hiyo na kushika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa wa ligi kuu nchini humo ikiachwa kwa alama 20 nyuma na vinara wa ligi hiyo ambao ni Liverpool.

Timu hiyo imeshinda michezo mitatu msimu huu kitendo ambacho kimewatia hofu mabosi wa Spurs ya kushushwa daraja ndani ya ligi kuu nchini Uingereza.

Sio Pochetino pekee aliyefungashiwa virago kwenye timu hiyo bali hadi benchi lake la ufundi lililowajumuisha Juses Perez, Miguel D’Agostino na Anton Jemenez.

 

Live: Magufuli akitatua kero za Wananchi Kibaigwa mkoani Dodoma
Vifo vya malaria vyapungua kwa asilimia 63