Bondia Mfilipino, Manny Pacquiao amefanikiwa kumpiga na kumchafulia rekodi ya kutopoteza pambano, aliyekuwa Bingwa wa Dunia wa Masumbwi ‘Uzito wa Welterweight’, Keith Thurman.

Pacquiao ambaye ana umri wa miaka 41, alianza mapema kuwaamsha mashabiki wake baada ya kumpiga chini Keith katika raundi ya kwanza.

Bingwa huyo wa masumbwi ambaye pia ni Seneta nchini kwake aliendeleza ubabe katika raundi tano za mwanzo, lakini Keith alirejea kuanzia raundi ya sita ya pambano na ikawa piga nikupige.

Hata hivyo, pambano hilo lililoziweka roho za mashabiki juu wakati wote lilimalizika katika raundi ya 12 na uamuzi wa jopo la majaji watatu lilimtaja Pacquiao kuwa mshindi.

Ushindi huo unaandika historia ya aina yake kwa Pacquiao ambaye wengi walikuwa wanamshauri kuachana na masumbwi kutokana na kuwa na umri mkubwa na majukumu ya kisiasa. Pia,  utaandikwa kwenye historia ya masumbwi kwa kuzingatia kuwa amempiga kijana machachari mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa anatajwa kwenye orodha ya wapiganaji bora zaidi watano duniani.

Keith, sasa anaandika rekodi ya kushindwa kwa mara ya kwanza na kupigwa chini kwa mara ya kwanza ulingoni akiwa na 29-1, 22 Kos.

Mkongwe Manny Pacquiao amebadili tarakimu kwenye rekodi yake na sasa inasomeka 62-7-2, 39 Kos.

Video: Urais unavyoitesa CCM, Lissu aingia"Vitani" rasmi
JPM amtumbua Makamba, Simbachawene, Bashe waula