Watu wanaosadikika kuwa ni magaidi wamevamia hoteli ya DusitD2 jijini Nairobi nchini Kenya na kulipua mabomu mawili pamoja na kufyatua risasi kadhaa.

Polisi nchini humo wameeleza kuwa washambuliaji sita waliojihami walivamia hoteli hiyo leo majira ya saa tisa mchana na kutekeleza mashambulizi hayo.

Magari yaliyokuwa kwenye eneo la maegesho ya magari katika hoteli hiyo yameteketea kwa moto na baadhi ya watu wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Aga Khan iliyoko karibu na eneo hilo.

 

Taarifa rasmi ya madhara yatokanayo na shambulizi hilo bado haijatolewa, lakini vikosi vya usalama pamoja na vikosi vya zima moto viliwasili kudhibiti eneo hilo na kurejesha usalama na utulivu.

Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini humo, George Kinoti amefika katika eneo hilo akiongoza vikosi vya wana usalama, kwa mujibu wa Citizen.

“Nilikuwa natembea karibu na jengo la hoteli, ghafla nikasikia milio ya bunduki na milipuko ya mabomu. Nikaona pia watu wakikimbia wakiwa wamenyoosha mikono juu na wengine wakakimbilia benki iliyokuwa karibu kujificha,” Reuters wanamkariri mama mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.

Al-shabab wakiri kuhusika shambulio Nairobi
BOT yafunga benki nyingine