Mbio za riadha za Boston Marathon zimefutwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 124 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Awali mbio hizo zilisogezwa mbele kutoka Aprili 20 kwenda Septemba 14 mwaka huu.

Mbio hizo ndio ndefu zaidi Duniani zimekuwa zikifanyika nchini Marekani tangu mwaka 1897, na hazijawahi kusitishwa hata kipindi cha vita vya Dunia.

Boston Marathon hushiriksha wanariadha 30,000 ambao wengi wao wanafuzu kushiriki mbio hizo kwa kukidhi viwango na ujumuisha wakimbiaji mahili kutoka katika mataifa mbalimbali.

Lawrence Cherono wa Kenya na Worknesh Degefa wa Ethiopia walishinda mbio za wanaume na wanawake mnamo mwaka 2019.

Troy Deeney akubali yaishe
Burudani ya soka kurejea Juni 13

Comments

comments