Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya Benchmark, Rita Paulsen ametangaza rasmi ujio mpya wa shindano la kusaka vipaji vya wasanii wa kuimba, ”Bongo Star Search” linalofanyika nchini Tanzania na kusema kuwa shindano hilo limezinduliwa rasmi hivyo wameomba watanzania kuwapokea vizuri kwani wamejiandaa vizuri na ujio mpya.

Ametaja kuwa usaili wa shindano hilo unatarajiwa kuanza rasmi Jijini Mwanza kuanzia Sepemba 22 hadi 23 na kuendelea Arusha Septemba 29 hadi 30 na kufanyika Mbeya Oktoba 6 hadi 7 na mwisho jijini Dar es salaam Oktoba 13 hadi 14.

Madam Rita amesema ujio wa msimu huu wa 9 ni ishara tosha kuwa shindano hili linamsimamo na limedhamiria kubadilisha maisha ya vijana wengi.

Amesema kuwa wote waliopita katika shindano hilo maisha yao yamebadilika sana kutokana na kutoa mfumo wa kubadilisha maisha ya vijana.

Aidha, Madam Rita ametoa wito kwa Serikali na kuiomba itoe mchango katika shindano hilo kwani linasaidia vijana kwa namna moja au nyingine kutokana na kutoa ajira na kuongeza pato la nchi kwa namna mbalimbali.

”Natoa wito kwa Serikali tunapenda kutambulika kuwa tunamchango fulani tunafanya kwa hiyo tupatiwe sapoti kuona na sisi  tunafanya kitu katika jamii kwani sisi ni kiwanda, tunatoa ridhaa kwa Serikali iangalie vizuri ishu ya muziki kwani vijana wakiwekewa mifumo sahihi wanaweza kujiajiri na kubadilisha maisha yao na kuongeza kipato cha taifa” Rita

Shindano hilo ambalo linaandaliwa na kampuni ya Benchmark Production chini ya Madam Ritha Paulsen na majaji wenziye Salama Jabiri na Master J, limewahi kufanikisha ndoto za wasanii wengi na kuibua vipaji vyao akiwemo Mwana Hip Hop Kala Jeremiah, Walter Chilambo, Baby Madaha, Peter Msechu na wengine wengi.

Chadema waiombea njaa CUF, "Kikitetereka sisi tutaimarika zaidi"
Jezi namba 10 kumsubiri mwenyewe Argentina

Comments

comments