Shirika la upelelezi la Marekani (FBI), limethibitisha kuwa mfungwa wa kosa la mauaji, Samuel Little amekiri kuwaua watu 93 miaka 40 iliyopita hivyo kuwa mhalifu hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Hadi sasa Little amehusishwa na mauaji ya watu 79 katika matukio 50 ya uhalifu aliyoanza mwaka 1970.

” Little tangu mwaka 2012 amekuwa akitumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya wanawake watatu weusi ambao baadhi yao walikuwa makahaba na watumiaji wa dawa za kulevya” wameeleza maofisa wa polisi.

Bondia huyo wa zamani alikuwa akiwapiga ngumi waathiriwa wake kabla ya kuwanyonga ili kuondoa ushahidi kuwa wameuawa kikatili.

FBI wamesema kuwa baadhi ya vifo hivyo havikuchunguzwa na maofisa wao, na vingine vilidhaniwa kutokana na ajali au sababu nyingine na miili mingine haikuwahi kupatikana.

Mchambuzi wa masula ya uhalifu, Christie Palazzolo amesema kwa miaka mingi, mtuhumiwa huyo aliamini hatawahi kujulikana kwasababu hakuna mtu aliye watafuta waathiriwa.

” Japo tayari ni mfungwa, FBI inaamini ni muhimu kuwatafutia haki waathiriwa ambao hawajathibitishwa.” aliongeza Palazzolo.

Maofisa wa usalama bado wanachunguza visa 43 vya mauaji aliyokiri kutekeleza na kuhusu visa vitano vya maiaji yaliyotekelezwa katika miji ya Kentucky, Florida, Lousiana, Nevada na Arkansas ili kusaidia utambuzi wa waathiriwa ambao hawajathibitishwa.

Awali FBI walisambaza michoro ya waathiriwa ambayo alichora akiwa gerezani katika juhudi za kuwatambua marehemu na pia walichapisha video fupi alizoeleza kwa kina jinsi alivyotekeleza mauaji hayo.

Aidha wameomba ushirikiano wa umma ili kumtambua mwanamke mwenye asili ya kiafrika kwa jina la Marianne au Mary Ann aliyeishi Miami na Florida mwanzoni mwa miaka ya 70.

 

 

Monalisa kuinua vipaji kwa watoto wa kike
Kiongozi aburuzwa nyuma ya gari kwa kutotimiza ahadi za uchaguzi