Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Boeing 787-8 Dreamlinner inatarajia kuanza safari zake za nje ya nchi ifikapo Julai mwaka huu.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika hilo, Josephat Kigirwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa safari hizo zitaanza Julai 17 mwaka huu ambapo sambamba na safari za India, pia Juni 28 wataanza kutoa huduma kati ya usafiri wa Johnsburg Afrika Kusini na Dar es salaam safari zikiwa mara tatu kwa wiki.

Aidha, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa mpango wao mahsusi wa kupanua huduma za shirika hilo nchini na nje ya nchi ambapo kwa sasa tayari wanatoa huduma katika mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo Kilimanjaro, Kagera, Kigoma, Mbeya, Mwanza, Dodoma,Tabora, Shinyanga na Zanzibar, ambapo amesema Kwasasa tayari (ATCL) inatoa huduma ya usafiri wa anga katika nchi 4 ambazo ni Burundi, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Hata hivyo, Kigirwa ameongeza kuwa kwasasa wanafanya tafiti mbalimbali na matayarisho ili kuanzisha safari zingine nchini ambapo wiki ijayo wataanza safari katika mkoa wa Iringa na tayari wako katika utaratibu wa kujiweka sawa kwaajili ya kuongeza huduma katika Viwanja vya Mpanda, Katavi, Mtwara, Ruvuma, Zanzibar na mkoa wa Tanga.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 25, 2019
Mwanamke Munira azinduka baada ya miaka 27 Hospital