Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), imeonekana kutekeleza dhamira ya kutibu ugonjwa wa nidhamu, ambao kwa kipindi kirefu umekua tatizo kubwa katika michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao:

 

Mchezo namba 178: Simba SC 2 – 0 Coastal Union 

Kocha wa Simba Steven VandenBroeck amepewa Onyo Kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi hiyo iliyochezwa Februari  01,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Mchezo namba 188: Simba SC 2 VS 1 Polisi Tanzania FC

Klabu ya Polisi Tanzania imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.1,500,000/=(Milioni Moja na Laki Tano) kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa  Februari 04,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Vile vile katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Sc Steven VandenBroeck ametozwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 41(12) kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Rugemalira atuma ujumbe kwa taasisi 9 kumuondoa kesi ya uhujumu
Mwamuzi wa Yanga Vs Lipuli FC afungiwa

Comments

comments