Bodi ya Filamu Tanzania imesema kuwa imeingia makubaliano maalum na Wema Sepetu ili aweze kutimiza masharti ya kuachiwa huru na kuendelea kufanya kazi za filamu.

Akizungumza Ijumaa katika mahojiano wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Filamu na Muziki ya Starline Films jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Bi. Joyce Fissoo alisema kuwa kwakuwa wanamhitaji muigizaji huyo, wanasubiri kuona namna atakavyotekeleza adidu za rejea alizopewa.

“Tunamhitaji sana Wema kwenye kiwanda cha filamu, lakini tunachukia sana maadili mabovu yanayoharibu kizazi chetu cha sasa ndio maana tumemfungia,” alisema Mama Fisso.

“Katika hatua za kufuatilia, tumempa terms of reference (hadidu za rejea), ni kitu gani afanye. Na tumempa miezi sita kutekeleza hivyo vitu ambavyo tunataka avifanye. Kwa kila siku ambayo atakuwa amefanya hivyo ambavyo tumemuelekeza na atatuletea journal ambayo itaeleza kila siku vitu ambavyo anavifanya,” aliongeza.

Aliongeza kuwa Wema anahitajika kwenye kiwanda cha filamu kwakuwa ana wadau wengi ambao wanategemea kufanya kazi naye kama sehemu ya ajira pamoja na mashabiki wanaotamani kuona kazi zake tena.

Bodi hiyo ilimfungia Wema kwa kipindi kisichojulikana, baada ya picha zinazomuonesha akiwa anapeana mabusu yanayopaswa kufanyika faragha na mwanaume mmoja ambaye alikuwa anamtaja kama mumewe mtarajiwa.

Video: Maneke aanika ya wasanii aliowafanyia kazi bure wakavimba na mamilioni
Tyson Vs Wilder laishangaza dunia, washindwa kupata mbabe

Comments

comments