Watu watano wanaotuhumiwa kufanya unyang’anyi wa bodaboda pamoja na kumbaka mwanamke aliyekuwa abiria wameuawa na Polisi jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya ‘GPS’ kuonesha walipo.

Kwa mujibu wa Polisi, bodaboda hiyo ilikuwa imefungwa kifaa maalum kinachowezesha kuonesha mahali ilipo (GPS/track), ambacho kiliwasaidia kuifuatilia watuhumiwa hao na kuwaua baada ya majibizano ya risasi.

Polisi wameleza kuwa muendesha bodaboda alikuwa anatoka eneo la Riverside kuelekea Lucky Summer lakini walivamiwa na watu watano wenye bastola.

Watu hao waliwanyang’anya vitu vyote, wakawafunga nyuso zao na kisha kumbaka mwanamke aliyekuwa abiria kabla ya kutokomea na pikipiki pamoja na simu, mkoba na fedha walizonyang’anya.

“Tulipata ripoti, na baada ya maafisa wa polisi kuwasiliana na kampuni iliyokuwa imeweka kifaa cha kung’amua bodaboda hiyo ilipo, tuliweza kuwafuatilia na kuwakuta karibu na kona kali ya Gitwamba karibu na Dandora,” taarifa ya Polisi imeeleza.

Imeeleza kuwa baada ya majibishano ya risasi, polisi waliwaua watuhumiwa wote waliokuwa na pikipiki nyingine pia.

Video: Mtandao kuchafua vigogo wanaswa, Lissu, Zitto vigeugeu
‘Kenya Airways’ yaandika historia ya safari ya kwanza Marekani