Nahodha wa klabu ya wekundu wa msimbazi  Simba, John Bocco amesema lengo la klabu hiyo kuelekea katika mchezo dhidi ya Majimaji ya Songea ni kushinda na kuhakikisha wanaweka heshima licha yakuwa tayari wamekwisha kabidhiwa kombe.

Mshambuliaji huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo cha East Africa Televisheni ambapo ameeleza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kwamba wapinzani wao wanapambana ili wasishuke daraja.

Bocco ameongeza kuwa licha ya kuteleza katika mchezo uliopita ambapo walifungwa na Kagera Sugar bao 1-0 wanachoangalia kwa sasa ni mchezo unaofuata na watahakikisha wanashinda.

Simba SC itashuka dimbani itashuka dimbani tarehe 28 mwezi Mei kupambana na Majimaji katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaopigwa mjini Songea.

 

Video: TCRA yatoa leseni kwa Online TV, Radio na Blogs
Masharti magumu yaliponza Kanisa, sasa kuburuzwa Mahakamani