Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter ameendelea kutoa msisitizo wa kutohusika na suala la ‘mlungula’ ambalo limelichafua shirikisho hilo baada ya shirika la upelelezi la nchini marekani FBI kuwakamata baadhi ya maafisa wake kwa tuhuma za rushwa.

Blatter amesema anashangazwa na wadau wa soka duniani kuendelea kumnyooshea vidole kwa kumjumuisha kuwa miongoni mwa maafisa wa FIFA ambao wanahusika na tuhuma hizo.

Rais huyo wa FIFA mwenye umri wa miaka 79, amesema hakuna haja kwa wadau wa soka kuendeleza kasumba ya kuamini jambo hilo na badala yake amewataka kutambua wazi hakuhusika na balaa hilo ambalo lilisababisha atangaze kuachia nafasi yake ya urais siku chache baada ya kuchaguliwa.

Katika hatua nyingine Blatter amesema yeye ni msafi na anatarajia ukweli wa mambo utafahamika siku atakapoingia katika pepo ya mwenyezi mungu.

Hata hivyo Blatter amesema laiti kama ingelikua na mamlaka makubwa duniani, angewapeleka jela wale wote wanaoendelea kumdhania alihusika na suala la mlungula kama ilivyo kwa maafisa wengine wanaoshikiliwa na FBI.

Blatter anatarajia kuachia madaraka ya urais wa FIFA wakati wa mkutano wa kamati kuu ya FIFA ambao utakutana siku chache zijazo, hatua mbayo itafungua milango ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo.

Mama Wa Chris Brown Amponza Mkwewe
Michuano Ya Wimbledon Open, Moto Wazua Taharuki Uwanjani