Bilionea na mmiliki wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos ambaye anatajwa kuwa mtu tajiri zaidi duniani hivi sasa, ametangaza kuyashindwa mapenzi na kuachana rasmi na mkewe, MacKenzie.

Bezos na MacKenzie wameishi ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 25, wakishirikiana pia katika masuala ya kibiashara lakini leo wameandika ujumbe wa pamoja kuieleza dunia kuwa maisha ya mapenzi pamoja yamewashinda licha ya kung’ang’ana mara kadhaa.

“Baada ya kipindi kirefu cha kuyasaka mapenzi na kuzuia majaribio ya kutengana, tumeamua kuachana rasmi na kuendelea kushirikiana kwenye maisha kama marafiki,” wawili hao wameandika kwenye ujumbe wa pamoja waliouweka Twitter leo.

Kampuni ya Amazon ambayo ilianzishwa miaka 25 iliyopita, wiki hii ilifanikiwa kuipiku thamani ya Kampuni ya Microsoft na kuwa kampuni yenye thamani zaidi duniani.

Jeff Bezos mwenye umri wa miaka 54, ametajwa na Bloomberg Billionaire Index kuwa mtu tajiri zaidi duniani, akiwa na utajiri wa $137 bilioni, ambao unazidi utajiri wa Bill Gates kwa $45bilioni.

MacKenzie, yeye ni mwandishi maarufu wa vitabu na mfanyabiashara. Baadhi ya vitabu maarufu alivyowahi kuviandika ni pamoja na The Testing of Luther Albright cha mwaka 2005 na Traps cha mwaka 2013.

Ulinzi mkali wazua jambo matokeo ya urais DRC
Meya wa mji wa Njombe awacharukia wakazi wa mjini kuhusu michango

Comments

comments