Klabu ya Arsenal wakati wowote huenda ikatangaza kukamilisha dili la usajili wa mlinda mlango kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Bayer Leverkusen Bernd Leno.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya Ujerumani,  mlinda mlango huyo tayari ameshaafikiana na uongozi wa Arsenal upande wa maslahi yake binafsi, na anatarajiwa kuwa mrithi wa Petr Cech.

Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery anaamini mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 26, atakua suluhisho sahihi katika lango la kikosi chake, baada ya kuona mapungufu kadhaa ya Petr Cech kwa misimu miwili mfululizo.

Leno ameitumikia Leverkusen kwa misimu saba mfululizo, huku akicheza michezo 233 ya ligi ya nchini Ujerumani (Bundesliga).

Kwa upande wa timu ya taifa ameshaitwa kikosini mara sita, lakini hakubahatika kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 kilichoteuliwa na kocha Joachim Loew kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi, licha ya kucheza fainali za kombe la mabara mwaka 2017.

Arsenbal tayari imeshakamilisha usajili wa mchezaji mmoja mpaka sasa, Stephan Lichtsteiner akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus.

 

Zaidi ya nusu ya bidhaa soko la Uganda ni ‘feki’
Kigwangalla ashangazwa na watanzania wanaosubiri kuajiliwa, 'Maisha hayakusubiri'