Vyama vya upinzani nchini Benin vyafungiwa kushiriki uchaguzi kwa kutofikia matakwa ya sheria mpya ya uchaguzi hivyo wananchi wanashiriki uchaguzi wa wabunge wapya bila wagombea wa upnzani.

Tume ya uchaguzi mwezi Machi mwaka huu ili idhinisha vyama vya kisiasa vinavyodaiwa kumuunga mkono Rais Patrice Talon, kushiriki uchaguzi baada ya kufikia masharti yaliyowekwa ya sheria mpya inayovitaka vyama kulipa ada ya dola 42,000 ili viruhusiwe kushiriki uchaguzi.

Katika nchi hiyo huduma ya intaneti imedhibitiwa huku mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma na kupokea ujumbe mfupi zikifungwa pia.

Wapiga kura milioni tano wamesajiliwa kushiriki zoezi la uchaguzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi linalojivunia kuwa na utawala thabiti wa kidemokrasia.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekosoa hatua ya kuzuiliwa kwa maandamano ya amani na kukamatwa kwa wanaharakati wa upinzani “Kuongezeka kwa visa vya kakamatwa na kuzuiliwa kwa wapinzani huenda kukazua ghasia nchini humo” amesema Francois Patuel kutoka shirika la Amnesty Iternational katika taarifa yake.

Kwamujibu wa shirika la habari la AFP, mfumo wa vyama vingi vya siasa ulibuniwa miaka mitano iliyopita nchini Benin na uchaguzi wa kwanza chini ya mafumo huo ulifanyika miaka ya 1990, ambapo vyama 20 viligombania viti 83 vya ubunge.

Rais Talon, ni mfanya biashara wa zamani aliyejulikana kama “mfalme wa pamba”, aliingia madarakani mwaka 2016.

Amesema marekebisho ya sheria ya uchaguzi yanalenga kuleta pamoja mamia ya vyama vya upinzani vilivyo na falsafa aina moja kwa lengo la kuimarisha mfumo wa siasa ya vyama vingi.

Aidha Talon alitia saini sheria ya kuwazuia wafanyakazi wa afya na wafanyakazi wengine wa serikali kugoma kwa zaidi ya siku 10.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mwanamitindo apoteza maisha stajini
Video: JPM afichua siri ya Askofu wa Katoliki, Kardinali Pengo aiangukia Serikali