Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Benard Paul ali maarufu kwa jina la Ben Pol afunguka na kusema kuwa Muziki wetu umepenya kikamilifu nchini Nigeria.

Ben Pol amesema kuwa muziki wetu umekuwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na zamani kiasi cha kuwafungulia mipaka wasanii wengi wa Tanzania hususani wanao hitaji kushilikiana na wasanii wa Nigeria na kuondokana na ugumu wa kuwapata wasanii wa Nigeria hasa pale wanapokua wanahitaji kushirikiana katika kazi.

‘’Muziki wetu kwa sasa umepenya nchini Nigeria kwa kiasi kikubwa na kiasi cha kuturahisishia sisi wasanii kuondokana na ugumu wa kuwashirikisha wasanii kutoka Nigeria, nasema hivyo kwakuwa mimi sikupata tabu kufanya kazi na Chidnma na tukafanikiwa kufanya kazi kwa wakati’’ amesema Ben Pol.

Idadi ya wasanii wa Nigeria ambao tayari wameshilikishwa na wasanii wa Tanzania inazidi kuongezeka kila siku na kutusaidia kuutangaza muziki wetu zaidi katika taifa lao na hawa ni baadhi ya wasanii ambao wamekwisha fanya kazi na wasanii kutoka Nigeria, Madee, Shetta, Diamond, Shilole, Ommy Dimpoz, Chege, Joh Makini na wengine wengi.

Ben pol amefikisha nyimbo mbili ambazo amefany na wasanii wa Nigeria kwani alimshirikisha Mr Eaz kwenye wimbo wa Phone na wimbo wake wa pili ni Kidume ambao amefanya na Chidnma.

Bavicha walivimbia Jeshi la Polisi
Mshike mshike kuendelea leo Ligi kuu Bara

Comments

comments