Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) limesema kuwa litaendelea na mpango wake wa kumuombea dua Tundu Lissu siku ya jumapili hii jijini Dar es salaam.

Wamesema kuwa zuio la Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa haliwahusu kwakuwa wamefuata taratibu zote zinazohitajika na kwamba wao hawafanyi maandamano kama alivyoeleza.

Aidha, jana Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilipiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) ili kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa yapo maeneo maalumu ya kufanya ibada hivyo ni muhimu wakayatumia hayo na si vinginevyo.

Jezi ya Tshishimbi yageuka Almas Songea
Ben Pol: Tumepenya kikamilifu Nigeria

Comments

comments