Baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) limewataka watanzania wote kwa ujumla hasa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika maombi ya Tundu Lissu kwa madai wamekamilisha taratibu zote za kisheria juu ya jambo hilo.

Hayo yamesemwa  na Katibu Mkuu (BAVICHA) Taifa, Julius Mwita kupitia ukurasa wao maalum wa Facebook wa chama hicho baada ya kupita siku ya moja tokea Kamishna Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa kuzuia kufanyika kwa maombi hayo yaliyopangwa kufanywa kwenye uwanja wa TP, Sinza Jijini Dar es Salaam kwa kuwa  hiyo siyo sehemu ya maombezi.

“Kupitia kamati ya maandalizi, BAVICHA inapenda kuwaambia Watanzania wote ambao watapenda kuhudhuria maombi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwa maandalizi yote muhimu yameshafanyika kwa ajili ya kuhakikisha shughuli hiyo ya kiimani inafanyika kama ilivyopangwa,”amesema Mwita

Aidha, Mwita amesema kuwa mpaka sasa wameshafuata taratibu zote za kisheria ambazo zimewaelekeza kutoa taarifa kwa mamlaka za kiserikali hususani Jeshi la Polisi.

Hata hivyo, Katibu Mkuu (BAVICHA) amesema maombi hayo yatafanyika katika uwanja wa Tip, Sinza darajani jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 8:00 mchana licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku kusanyiko hilo.

Nyalandu amtembelea Lissu Nairobi
Watu 20 washikiliwa na polisi kwa tuhuma za ushoga

Comments

comments