Kijana mmoja mwenye umri wa mika 25, amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi na Polisi alipo teka Ndege iliyobeba abiria 148  ikitokea Bangladesh kuelekea Dubai ili aweze kuongea na Waziri mkuu wa nchini humo.

Raia huyo wa India mjini Bangladeshi Mohammad Palash Ahmed, alifikwa na umauti juzi kutokana na majeraha ya risasi aliyoyapata kwa kupuuza amri ya polisi waliomtaka aweke Bastola yake chini.

Rubani wa ndege alilazimika kutua kwa dharula baada ya abilia wake kutekwa na kijana anayetaka kuongea na waziri mkuu aliyekuwa kwenye ziara mjini Chittagong.

Taarifa za awali zilizotolewa na polisi zinaonesha kuwa kijana huyo alidhaniwa kuwa na matatizo ya akili na alihofiwa kufyatua risasi endapo hata dhibitiwa, hivyo iliwalazimu polisi kumdhibiti na kupelekea kupoteza maisha.

Kamishna wa Polisi Kusum Dewan, amesema  kwa uchunguzi uliofanywa imebeinika kuwa, Ahmed alikuwa ameshika bastola ya kuchezea watoto “toy gun” ambayo haiwezi kumdhuru binadamu, na alitumia kama njia ya kufanikisha lengo lake la kuongea na waziri mkuu ili anusuru ndoa yake.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa kiwanja cha Ndege Sarwar-e-Zaman, amesema kuwa “sababu iliyomfanya kijana huyu kuteka abiria wa ndege ni kuwa anamatatizo na mke wake na anataka kuongea na waziri mkuu, Sheikh Hasina ili amsaidie.

Bado uchunguzi wa juu ya njia alizotumia kuingia kwenye ndege na bastola hiyo licha ya kuwa na ukaguzi mkali na wa taknolojia ya juu unaendelea katika kiwanja hicho, na ulinzi umeimarishwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Serikali kusimamia maadili ya Polisi
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 27, 2019